Mgombe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 103,357 sawa na asilimia 96.6 ya kura zote zilizopigwa jimboni hapo.
Awali vyama vya siasa 16 vilijitokeza kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo lakini vyama 14 vilikosa sifa na baadhi yao kushindwa kurejesha fomu mpaka muda ulipokwisha huku CCM na ACT Wazalendo vikikidhi vigezo na kugombea.
Akitangaza matokea hayo, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Mwalimu Lino Pius amesema idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 165,418 lakini waliopiga kura walikuwa 107188.
Asema kati ya kura hizo idadi halali ya kura zilizopiga zilikuwa 106,945, idadi ya kura zilizokataliwa zilikuwa kura 243, huku mgombea wa ACT Wazalendo Julius Nkwabi Mabula akipata kura 3588 sawa na asilimia 3.4.
Hata hivyo, Mwalimu Mwageni amesema kuwa, mpaka anatangaza matokea hayo hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika vituo vya kupiga kura, hivyo uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na wananchi walijitokeza vile ilivyowezekana.
Na hizi ni Baadhi matukio ya picha wakati wa Kampeni
Mtaa Kwa Mtaa ,Hatua Kwa Hatua Uvccm Taifa wakati wakiendelea kupambania Kura za Chama cha Mpinduzi CCM na kuelezea kwa Wananchi namnagani Ilani inavyoendelea kutekelezwa
Na Abdul B Ramadhani
0 Comments