MORRISON SASA ADHABU YAKE IMEISHA, GOMES ACHEKELEA

DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kurejea kwa kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison ni miongoni mwa vitu ambavyo vinampa matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

Oktoba Mosi ilikuwa ni mara ya kwanza kwa msimu wa 2021/22 mabingwa hao watetezi wanapata ushindi hivi karibuni baada ya kusota kwenye mechi zao mbili za ushindani.

Septemba 25 walinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ilikuwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2021/22 walilazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United, Uwanja wa Karume Mara.

Ushindi wao ilikuwa ni bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri Dodoma na mtupiaji alikuwa ni Meddie Kagere kwenye mechi zote tatu Morrison alikuwa jukwaani kwa sababu alipata adhabu ya kufungiwa mechi tatu kutokana na kitendo chake cha kuvua bukta kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

Jambo hilo lilifanya afungiwe mechi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) tayari adhabu yake imeisha anarejea uwanjani kuonyesha makeke yake.

"Michezo mitatu iliyopita ilikuwa na ushindani mkubwa na kila timu imeonyesha inahitaji jambo nasi tumejifunza na imekuwa faida kwetu katika hilo ninaweza kusema kwamba tuna mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Pia nina furaha kuona kwamba nitakuwa na nafasi ya kumtumia Bernard Morrison kwenye mechi zetu zijazo hivyo ni jambo la furaha kwetu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments