Recent-Post

ORODHA YA NCHI AMBAZO WANANCHI WAKE WANAKULA NYAMA ZA MBWA NA PAKA

TAIWAN imepiga marufuku uuzaji na ulaji wa paka na mbwa kufuatia visa kadhaa vya ukatili dhidi ya wanyama na kuzua ghadhabu ya umma.

 

Sheria mpya ya kulinda wanyama imeweka adhabu ya faini pauni 6,500 kwa yule anayepatikana akiuza, kula au kununua nyama hiyo. Wanaopatikana wakiwadhulumu wanyama nao watapigwa faini ya pauni 52,000 na miaka miwili gerezani.

 

Taiwan ndilo taifa la kwanza kuweka marufu hii Barani Asia. Sheria mpya inanuia kukabili baadhi ya imani kuhusu ulaji mbwa. Kwa mfano kuna baadhi wanaamini kumla mbwa mweusi wakati wa msimu wa baridi kunamsaidia mtu kupata joto mwilini. Sheria hii imeungwa mkono na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, ambaye ana mbwa watatu na paka wawili.

 

Ulaji wa paka na mbwa umeendelea kupungua wakati jamii ikibadilisha jinsi inavyoshughulikia wanyama wanaofugwa nyumbani. Shirika linalotetea mslahi ya wanyama ‘Humane Society International’, limetaja mataifa ambayo yana desturi ya kula mbwa na paka.

 

Haya ni pamoja, Thailand, Laos, Vietnam, Cambodia na jimbo la Nagaland nchini India. Aidha desturi hii iko katika nchi za ChinaKorea Kusini na Ufilipino.

 

CHINA

Licha ya kutokuwepo na takwimu rasmi, China inaaminika kuongoza duniani katika ulaji na uuzaji wa mbwa na paka. Kila mwaka karibu mbwa na paka milioni 10 wanaaminika kuchinjwa nchini China. Shirika linalotetea maslahi ya wanyama linasema wanyama wengi wanaibwa wakati wakionekana barabarani bila wamiliki wao.

 

China inaongoza duniani kwa ilaji wa nyama ya Mbwa na PakaMteja akimkagua mbwa katika soko la Yulin China. Katika mji wa Yulin huko China mwezi Juni husherekea sherehe maalum ya mbwa na paka. Inakadiriwa mbwa na paka 10,000 huchinjwa mwezi huu kwa tamasha hiyo. Mwaka uliopita sherehe hizo zilikumbwa na maandamano kupinga kuwajicha mbwa na paka.

 

KOREA KUSINI

Nchini Korea Kusini, nyama ya mbwa ni maarufu sana kiasi cha kitoweo chake kupewa jina la ‘Gaegogi’. Inaaminika taifa hilo lina mashamba 17,000 yanayowafuga mbwa na kuuzwa kuwa chakula. Hata hivyo shinikizo za mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama zimeanza kuzaa matunda.

 

Korea Kusini imefunga soko kubwa la kuuza mbwaMchuzi wa nyama ya Mbwa Korea Kusini. Hapo mwezi Februari, soko kubwa zaidi la mbwa lilifungwa katika eneo la Seongnam, kabla ya Korea Kusini kuandaa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

 

VIETNAM

Takriban mbwa milioni tano wanaaminika kuchinjwa na kufanywa kitoweo nchini Vietnam kila mwaka. Ongezeko la wateja wa nyama hii limepelekea kuwepo na biashara ya magendo ya nyama ya mbwa katika nchi jirani za Thailand, Cambodia na Laos.

 

Mataifa ya Asia yameanza sheria kuthibiti ulaji wa nyama ya Mbwa na Paka. Mbwa wa Thailand ambao wanauzwa Soko la Vietnam. Shirika linalotetea haki za wanyama la ‘Asia Canine Protection Alliance’, limeshinikiza serikali kujaribu kumaliza biashara ya nyama ya mbwa.

 

Shirika hilo limesema lina ushahidi kwamba nyama ya mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu,na huenda ikasabaisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa miongoni mwa watu wanaokula nyama yake. Limetaka biashara hiyo kumalizwa katika mataifa ya ThailandLaos na Vietnam.

Post a Comment

0 Comments