Recent-Post

Rais Samia aanza ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 15,2021 kwa ajili ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2.Mhe. Rais Samia yupo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhe. Makame Mbarawa pamoja na baadhi ya watendaji Wakuu wa Wizara hiyo mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro. (PICHA NA IKULU).

Post a Comment

0 Comments