Recent-Post

Samia aweka jiwe la msingi jengo la mionzi KCMC

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 ameweka jiwe la msingi katika jengo la mionzi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC), ili kuendelea na ujenzi.

Kukamilika kwa jengo hilo kutawezesha wagonjwa wa saratani, wanaohitaji huduma hiyo kuipata kwa karibu wakiwa mkoani humo.

Pia, Rais Samia amezindua mnara wa Jubilee na kushiriki maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

Katika maadhimisho hayo, ibada ya shukrani  inaongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ambapo  kauli mbiu  ya maadhimisho hayo, ni kuendeleza na kuboresha misingi na mazingira ya utoaji wa huduma za tiba, mafunzo na tafiti kwa miaka 50 ijayo.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria maadhimisho hayo wakiwemo Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu, Waziri wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda, Waziri wa ujenzi , uchukuzi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na Naibu waziri wa afya, Dk Godwin Mollel pamoja na wabunge wote wa mkoa wa Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments