Recent-Post

SERIKALI YATOA BILIONI 6.3 KUKARABATI VIVUKO NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya pamoja na wananchi wakazi wa Msangamkuu na Msemo wakishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MAFANIKIO baada ya kukipanda ambapo kiliwapeleka upande wa Msangamkuu na kurudi Msemo baada ya kupokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70 na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Msemo Shangani katika kivuko cha Msangamkuu.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akimuonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti wakati walipokuwa wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO ambacho kimepokelewa leo na Mkuu huyo wa Mkoa. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70 na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wakijadiliana jambo mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kupokea rasmi kivuko cha MV. MAFANIKIO katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo la Msemo Shangani katika kivuko cha Msangamkuu. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kushoto akimuonyesha kitu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wakati walipokuwa wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO mara baada ya kukipokea rasmi mapema leo katika hafla fupi iliyofanyika Mkoani Mtwara. Mbele yao ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Mkurugenzi wa vivuko wa Wakala huo Mhandisi Adelard Kweka.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti katikati, mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto wakishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MAFANIKIO baada ya kukipokea mapema leo. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70 na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akikata utepe kuashiria kukipokea rasmi kivuko cha MV. MAFANIKIO baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Msemo Shangani katika kivuko cha Msangamkuu.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (MTWARA)

…………………………………………………………

Na. Alfred Mgweno (TEMESA MTWARA)

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, chini ya Wakala wa Ufundi na

Umeme Tanzania (TEMESA) imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwa

mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa ajili ya kuvifanyia ukarabati mkubwa

vivuko nchini ambavyo vimefikia muda wake wa ukarabati.

Hayo yamebainishwa leo wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. MAFANIKIO

kilichorejea kutoa huduma Mkoani Mtwara baada ya kukamilika kwa

ukarabati wake uliochukua takribani miezi miwili na nusu.

Akizunguma na wananchi waliofika kushuhudia tukio la upokeaji wa kivuko hicho lililofanyika katika eneo la Msemo Shangani Mjini Mtwara katika kivuko cha Msangamkuu – Msemo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amesema ni utaratibu wa kawaida kwa Serikali kuvifanyia vivuko ukarabati kila inapopita miaka minne hadi mitano ili kuviwezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na hivyo kivuko cha MV. MAFANIKIO wakati wake wa kufanyiwa ukarabati mkubwa ulifikia na hivyo ikawalazimu TEMESA kukiondoa ili kirejee kikiwa kiko salama na tayari kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo.

‘’wote tunafahamu kati ya Msangamkuu na Msemo ni takribani mita 700, kwa kivuko hiki tunatumia dakika takribani tano mpaka kumi, lakini ukiondoa kivuko hiki barabara ni kilometa 29, barabara ya changarawe kutoka hapa mpaka Msangamkuu na unatumia zaidi ya saa moja mpaka saa moja na nusu kwa barabara kwahiyo mnaweza kuona ni kiasi gani kupatikana kwa kivuko hiki baada ya matengenezo makubwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wetu wa Msangamkuu katika swala la usafiri na usafirishaji’’. Alisema Mkuu wa Mkoa ambapo alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha ukarabati huo.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, akizungumza katika hafla hiyo fupi amesema ukarabati wa kivuko cha MV. MAFANIKIO umefanywa na kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Ltd. Boat Yard ya jijini Mwanza kwa gharama ya TZS. 493,609,357.70 (pamoja na ongezeko la kodi-VAT).

‘’Baadhi ya kazi zilizofanyika katika ukarabati huu ni pamoja na Kuweka deki mpya ya magari, kuweka milango mipya miwili (2-New ferry ramps), kuweka ramp lifting cylinder cover mpya, kutengeneza mifumo ya steering, propulsion pamoja na injini na kupaka rangi kivuko chote.’’ Alisema Mtendaji Mkuu na kuongeza kuwa Gharama zote za ukarabati wa kivuko hiki zimegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhandisi Maselle amevitaja vivuko vitkavyofanyiwa ukarabati kwa mwaka huu

wa fedha wa 2021/2022 kuwa ni MV. Kitunda (Lindi), MV Tanga (Pangani

Tanga), MV Kazi na MV magogoni (Dar es salaam), MV Ruhuhu (Ruvuma) pamoja na vivuko vinavyofanya kazi kwenye ziwa Victoria ambapo amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwa ajili ya ukarabati wa vivuko hivyo.

Aidha, Mhandisi Maselle pia ameishukuru Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kuendelea kuuamini Wakala na kuahidi kuendelea kutunza kivuko hicho pamoja na vivuko vingine kwa kuvifanyia matengenezo kama inavyotakiwa ili viweze kudumu na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kivuko cha MV. MAFANIKIO kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari sita sawa na tani 50 na kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara.

Post a Comment

0 Comments