SIMBA YATAMBA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA


 UONGOZI wa Simba SC umetamba kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kuiwakilisha vema Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, Oktoba 17, mwaka huu.


Simba imeanzia hatua ya kwanza ya michuano hiyo ambapo mechi ya kwanza itachezwa nchini Botswana, kisha marudiano Dar, Oktoba 22, mwaka huu.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema: “Kama uongozi tunaendelea kufanya maandalizi ya kikosi chetu kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, ni jambo zuri kuwa tunauelekea mchezo huu tukiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Dodoma Jiji kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.


“Bahati nzuri kwetu ni kwamba wachezaji wetu wana uzoefu na mashindano haya, lakini ubora wa kikosi tulichonacho ni sababu tosha ya kufanya vizuri.”


Msimu uliopita, Simba iliishia robo fainali ya michuano hiyo, huku ikiwa ni mara ya pili kwa misimu ya karibuni baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018/19.


Kwa sasa kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi kwa msimu wa 2021/22 licha ya ligi kusimama kutokana na timu za taifa kuwa na kazi kwenye majukumu ya kusaka tiketi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Simba kwa sasa ni pamoja na Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude.

Post a Comment

0 Comments