TIMU YA MAWAZIRI NANE YATUA RASMI SINGIDA NA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWENYE MAENEO YENYE MIGOGORO YA ARDHI

 

Timu ya Mawaziri nane wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakipokeleqa na viongozi wa Mkoa wa Singida baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini hapa tayari kwa mkutano kwa ajili ya kutoa matokeo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 920.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuviakimkabidhi ripoti ya utatuzi wa migogoro hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimuelekeza jambo Bibi Asha Mkaku mkazi wa mtaa wa Mwankoko mkoani Singida wakati wa ziara ya timu ya Mawaziri wa Kisekta ilipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mwankoko. 
Moja ya Tanki kwenye mradi wa visima vya maji katika mtaa wa Mwankoko likikaguliwa.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Katibu Mkuu Wizara ya ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza kwenye mkutano huo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza kwenye mkutano huo.
Waziri wa Maji Juma Awesso akizungumza kwenye mkutano huo.
Naibu Waziri TAMISEMI .David Silinde akizungumza kwenye mkutano huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mary  Masanja akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akizungumza kwenye mkutano huo.
   


Na Dotto Mwaibale  Singida

 

MAWAZIRI nane wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi hatimaye wameanza rasmi ziara ya kutembelea mikoa 10 ikiwemo Singida kwa ajili ya kutoa matokeo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 920.

Wakiwa mkoani Singida leo Oktoba 8, 2021 Lukuvi alisema ziara hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusiana na migogoro ya  matumizi ya ardhi kwenye vijiji na mitaa 12 ambavyo wananchi wake walivamia maeneo ya hifadhi za misitu, mashamba na mifugo ndani ya Mkoa wa Singida.

" Tuneleta timu ya kufanya tathmini, kiweka alama na mipaka inayoonekana ili kujua kiwango cha ardhi kinachotakiwa kutumiwa na wananchi waliopo katika maeneo hayo," alisema Lukuvi na kuongeza;

"Suala la kuwa na wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi je wabaki au wasibaki hilo limeshamalizwa na Mheshimiwa Rais Samia kwamba wabaki wasiondolewe."

Alifafanua mantiki ya ziara hiyo alisema katika kujua wananchi hao wanabakije suala la uungwana linahitajika ambalo ni wao kujiridhisha kwa kufanya tathmini kwa ardhi waliovamia ili ardhi itakayobaki ilindwe kwa mujibu wa sheria.

Ziara hiyo imekuja kutokana na baadhi ya hifadhi kuonekana kukosa sifa na Serikali kuamua wananchi wabaki katika maeneo hayo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge alisema, ofisi yake sasa itahakikisha inasimamia pamoja na kuifatualia migogoro yote ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka katika wilaya na vijiji ili kumaliza kabisa migogoro ya ardhi.

Wakiwa katika Manispaa ya Singida Mawaziri hao wametembelea eneo la Mwankoko  lenye mgogoro ulioanza mwaka 2016 kati ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini hapa (SUWASA)  na wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia waliyolipwa na Serikali ili kupisha utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Mwankoko ambapo baada ya Mawaziri kusikiliza pande zote mbili, Mwenyekiti wa Kamati wa Mawaziri wa Kisekta ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemwagiza Mthamini Mkuu wa Serikali kufika mkoani hapa siku ya Jumatatu ya wiki ijayo ili kufanya uchunguzi na kujua ukweli kuhusu malalamiko hayo.

Mawaziri hao wa kisekta waliokuwa kwenye ziara hiyo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mazingira, Utalii, Ulinzi na Maji.

Hata hivyo kwa mujibu wa Lukuvi timu hiyo mawaziri baada ya Singida inatarajia kuendelea na ziara hiyo kwa awamu ya kwanza katika mikoa mingine ya Tabora, Manyara, Mbeya, Morogoro, Geita, Mara, Dar es Salam na Pwani. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments