Wanawake wahamasishwa kuchanja, kushiriki sensa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya CCM Dar es Salaam, Frolence Masunga amewahimiza wanawake nchini kupata chanjo ya Uviko-19 ili afya zao ziwe salama.

Ameeleza hayo jana Jumapili Oktoba 24, 2021 wakati wa kilele cha kongamano la siku saba la kuwajengea uwezo wanamke kuhusu sheria za fedha, malezi ya watoto, kujitambua, kujielewa yeye ni nani na akipewa nafasi ajue anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii.

Kongamano hilo, lilikuwa ni sehemu ya kuendeleza yaliyoachwa na aliyekuwa mchungaji wa kanisla hilo, marehemu Dk Getrude Rwakatare aliyeanzisha mpango huo wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala mbalimbali.Lilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni.

“Chanjo ni hiari sio lazima. Mimi naweza nikachanja au nimeshachanja, lakini mwanamke akipata tatizo kama hili, familia itapata shida kubwa.Ni vyema wanawake tukachanja ili kuwa salama katika maisha yetu,” amesema Masunga.

Mbali na hilo, amewataka wanawake nchini kujitokeza katika mchakato wa sensa na makazi ya watu utakaofanyika kuanzia Agosti mwakani, akisema ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

“Tunakwenda kwenye sensa mwakani, nimeambiwa hapa kanisani kuna wanawake 600, nawaomba tujitokeza ili kuunga mkono hatua hii. Pia nawashukuru viongozi wa Mlima wa Moto kwa kuendeleza kwa ufanisi maono ya Dk Rwakatare,” amesema Masunga.

Mchungaji kiongozi wa Mlima wa Moto, Rose Mgeta amesema kongamano hilo, limefanyika kwa mafanikio makubwa na kuwashuruku waliojitokeza kushiriki mchakato.Alisema limesaidia pia kuwasaidia kina mama wasiojiweza.

Mlezi wa Mlima wa Moto, Dk Rose Rwakatare amesema kongamano la siku saba limefikia hitimisho huku akiwashukuru walimu na wazungumzaji katika semina hiyo.

“Washiriki wametoka na kitu tofauti na hapo awali, sasa tutaendelea na kogamano hili kila mwaka, maono ya Dk Rwakatare yataendelea sio kongamano hili pekee bali mengine tofauti na hili,” amesema a Dk Rose.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments