Watendaji wa kata waahidi kusimamia fedha za Uviko-19

Watendaji wa kata katika wilaya ya Sengerema wameahidi kuzisimamia fedha za Uviko-19 zilizotolewa na Shirika la Fedha duniani (IMF) kama alivyoelekeza Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.

Ofisa mtendaji, kata ya Bulyaheke, Jonathan Kuditha amesema wamejipanga kusimamia idara ya jamii itakayotekelezwa kwenye kata zao ili kutokomeza Uviko-19, ugonjwa unaoitesa dunia kwa sasa.

“Tumesikiliza maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa aliyoyatoa kwa wakuu wa mikoa pamoja na makatibu wakuu kuhusu usimamizi wa fedha hizo, kwamba tunanapaswa kusimamia vema na kutekeleza miradi ya afya, elimu na maji.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Buchosa, Paul Malala amesema katika fedha hizo wao watajenga vyumba vya madarasa 142, kati ya hivyo, sekondari madarasa 128 na msingi madarasa 14 ambavyo vitasaidia upungufu wa madarasa kwenye halmashauri hiyo.

Baadhi ya wananchi wilayani Sengerema wamepongeza hatua ya Serikali kwa kutumia fedha hizo kwa ajili ya kutekeleza huduma za jamii ambayo itawasaidia wananchi juu kupambana na Uviko-19.

Mmoja wa wananchi wilayani humo, Anastania John amesema miradi ya afya, elimu na maji itakayotekelezwa Wananchi watakuwa wamepata elimu kubwa juu ya kujikinga na Uviko-19.

Wakati huohuo, mwitikio wa chanjo ya Uviko-19 kwenye halmashauri ya Sengerema umeongezeka ambapo watu 4762 wamepata chanjo hiyo wakati shughuli hiyo ikiwa bado inaendelea ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

Mganga mkuu wa halmashauri ya Sengerema, Saumu Kumbisaga amesema timu ya afya imepiga kambi vijiji kutoa elimu na kutoka chanjo ya Uviko-19.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments