Waziri Makamba akaribisha mawazo sekta ya nishati

Waziri wa Nishati January Makamba amekaribisha ushauri na mawazo ya wadau ili kuboresha sekta hiyo huku akiahidi kuwa wamejipanga kufanya makubwa.

Amesema na kufahamu kuwa kazi iliyo mbele yake sio nyepesi ana imani na timu yake kwa kuwa ina uwezo wa kufanya mabadiliko.

Makamba ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Oktoba 15 jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la Nishati na Madini lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Makamba amesema katika kipindi cha mwezi mmoja alichoingia kwenye wizara hiyo wameanza kuyafanyika kazi mambo 10 kwa lengo la kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyo.

Miongoni mwa mambo hayo ni kusimamia biashara ya mafuta na kuhakikisha inakuwa tulivu na nishati hiyo inapatikana kwa bei nafuu.

Post a Comment

0 Comments