YANGA KUSHUKA UWANJANI LEO MBELE YA JKU SC

LEO Oktoba 10 kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kinatarajiwa kujipima ubavu na timu ya JKU  SC katika mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Wachezaji ambao wamebaki kambini Dar katika kijiji cha Avic Town ikiwa ni pamoja na Mayele, Abdul Shaibu, 'Ninja', Paul Godfrey, 'Boxer' watakuwa na kazi ya kujiweka sawa na kuonyesha uwezo wao.

Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku na utakuwa live Azam TV.

Kwa upande wa kiingilio kwenye mchezo huo mzunguko ni buku tatu pekee, (3,000) na VIP 5,000,(buku tano).

Mastaa ambao wapo kwenye majukumu yao ya taifa ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum hawa hawatakuwepo kwenye kikosi cha leo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments