Recent-Post

ADEL ZRANE AWAGUSA WENGI KUONDOKA SIMBA SC

Aliyekuwa Kocha wa Viungo wa Simba SC, Adel Zrane alipokuwa kwenye moja ya majukumu ya hiyo kabla ya kuondoka.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KWA MASIKITIKO! Kama alivyoandika aliyekuwa Kocha wa Viungo wa Klabu ya Simba SC, Adel Zrane ikiwa ni siku chache baada ya kufika makubaliano ya pande zote mbili kwa baadhi ya Wataalamu wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, kutokana na mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho.

Moja ya watu walifika makubaliano ya kuvunja mkataba na Simba SC ni Aliyekuwa Kocha Mkuu, Mfaransa Didier Gomes Da Rosa, Aliyekuwa Kocha wa Makipa, Mbrazil Milton Nienov na Aliyekuwa Kocha wa Viungo, Mtunisia Adel Zrane wote kwa pamoja waliachana na timu hiyo baada ya kutupwa nje kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2021-22.

Kuondoka kwa Kocha Adel Zrane kumewasikitisha wadau wengi wa Soka nchini, hususani kutokana na utashi wa Mtaalamu huyo katika mazoezi ya Viungo kwa Wachezaji wa Simba SC, si kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo (Warm Up), kupasha misuli kwa Wachezaji wanaotaka kuingia kwenye mchezo husika (Substitution) na hata wanapoingia Uwanjani pindi watokapo mapumziko (Half Time).

Baadhi ya Mashabiki na Wadau wa Soka wamesikitishwa sana kuondoka kwenye Benchi la Ufundi, Mtaalamu huyo kama alivyosikitishwa yeye binafsi na kuandika kwenye ukurasa wake rasmi wa ‘Instagram’ ujumbe ulioashiria kuwaanga Wanasimba na Watanzania kwa ujumla katika kipindi cha misimu minne aliyokuwepo Tanzania.

Adel Zrane ameandika, “Kwa masikitiko makubwa naondoka nchi niipendayo Tanzania, yametimia muda umekwisha. Naipenda Tanzania nawatakia kila la heri watu wote na utawala wake.  Tanzania itakuwa kimbilio langu la kwanza kwa likizo, nawapenda wote na asante kwa misimu yote 4 iliyopita.  Mmekua familia yangu ya pili nawapenda na kuwaheshimu wote”.

Baadhi ya wadau hao wa Soka nchini, wanaamini Kocha Adel Zrane alifanya kazi iliyotuka kwa Benchi la Simba SC na Wachezaji kwa pamoja katika kipindi hicho cha misimu minne ya mafanikio ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa Klabu ya Simba SC wakati wengine wakimkingia kifua Kocha aliyeachwa Didier Gomes.

Benchi la Ufundi la Simba SC lilivunjwa kwa baadhi ya Wataalamu kufutwa kazi, huku Kocha raia wa Burundi, Thierry Hitimana na Mtanzania Suleiman Matola wakibaki kwenye Benchi hilo na hivi karibuni ameletwa Kocha mpya kutoka Hispania, Pablo Franco Martin akitajwa kuleta Soka la Tiki Taka katika ardhi ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments