Bashungwa Aungana Na Rais Samia 'Kuupiga Mwingi'Tembo Warriors Ishinde CANAF 2021.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amesema Serikali imeshakamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kuanza mashindano ya Mataifa ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu (CANAF) yanayotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam

Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari leo, Novemba 26, 2021 akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulamavu nchini, Moses Mabula, Mhe. Bashungwa amesema Tanzania imepewa heshima ya kuandaa mashindano hayo kutokana na uzoefu na umakini katika kuandaa mashindano ya kimataifa ya michezo.

“Ndugu zangu Waandishi tunafurahi kuona kuwa nchi yetu imeendelea kuratibu mashindano mengi ya kimataifa, hii inatokana na uzoefu katika nyanja mbalimbali  ya kuandaa mashindano haya”. Amefafanua Mhe. Bashungwa.

Aidha, Mhe. Bashungwa ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa kutoa shilingi milioni 150 jana ili zisaidie kwenye maandalizi ya mashindano ya Timu ya Soka ya Taifa ya Walemavu ya Tanzania “Tembo Warriors”.

 Pia amesema kwenye mashindano haya Tanzania imechukua tahadhari zote za ugonjwa wa Uviko-19.

Naye Mabula ameishukuru serikali kwa  kuisaidia  timu hiyo na  kuihakikishia Serikali kufanya vizuri katika mashindano hayo ambapo amesema  kwa mara ya kwanza  mashindano haya yatahusisha  kufuzu kuelekea  kombe la dunia  tofauti na awali.

Wakati huo huo, Mhe. Bashungwa amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuitangaza tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.  Kufuatia hatua hii muhimu.

Ametoa wito kwa  wapenzi, wadau na asasi mbalimbali za  Kiswahili hapa nchini kuongeza mbinu za Kisasa za kukitumia na kukitangaza Kiswahili duniani.

 “Tuhamasishe wadau wa fani nyingine kama vile za Uhandisi, Sheria na Habari ili wakipende Kiswahili na kukitumia katika shughuli zao”. Ameongeza Mhe. Bashungwa.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments