CCM YAMTEUA EMMANUEL SHANGAI KUWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NGORONGORO


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imekutana katika kikao maalum Jumapili 7 Novemba, 2021 Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Ndugu Emmanuel Lekishon Shangai kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ngorongoro katika uchaguzi

mdogo utaofanyika tarehe 11 Disemba, 2021 kufuatia kifo cha Marehemu William Tate Ole Nasha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kamati Kuu imewateua Ndugu Gulamhafeez Abubakar Mukadam na Ella's Ramadhani Masumbuko kugombea kiti cha Umeya katika Manispaa ya Shinyanga Mjini.

Katika hatua nyingine kamati kuu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya ujenzi wa taifa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kamati Kuu imempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuingia madarakani kuwa Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuendeleza mshikamano, kulinda tunu ya Umoja, Amani, utulivu sambamba na utekelezaji makini na imara wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments