CHAMA CHA MAPINDUZI MSINGI WAKE NI SHINA,BILA UIMARA WA SHINA HAMNA UIMARA WA CHAMA-KATIBU MKUU CCM

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo ametoa pongezi za dhati kwa shina namba 1, Tawi la Milupwa, Misunkumilo kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama.


Katibu Mkuu ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi yenye lengo la kukagua uhai wa Chama pamoja na kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

“Shina hili limevunja rekodi ya mashina yote ambayo nimeyatembelea toka nimeanza ziara nilipoteuliwa Ukatibu Mkuu, Shina hili linawanachama 207 idadi hii ni kubwa kweli kweli hongereni” amesema Katibu Mkuu.

Chongolo amewaambia wakazi wa shina namba 1 kuwa Chama Cha Mapinduzi msingi wake ni shina na bila mashina imara hamna uimara wa Chama chetu.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM alioneshwa kuvutiwa na Shina hio linaloongozwa na Dorothea Raphael.

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Ndugu Sebastian Kapufi amempongeza Katibu Mkuu huyo wa CCM kwa kuonyesha kwa vitendo maana halisi ya Uongozi na kuahidi kuendelea kushirikiana na wananchi bega kwa bega ambapo amesema kuwa atashirikiana na wananchi katika sughuli zote za maendeleo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo juu ya ujenzi wa mradi wa Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia nafaka kutoka kwa Mhandisi Mkazi Ndugu Musa Jumanne (kulia)vilivyopo Mpanda mkoani Katavi. (Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shina namba 5 Ndugu Noel Tayari (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye kikao cha Shina hilo lililopo Tawi la Kilimani kata ya Nsemulwa,Mpanda mkoani Katavi. (Picha na CCM Makao Makuu)
Pichani ni sehemu ya wakazi wa Shina namba 5, Tawi la Kilimani kata ya Nsemulwa,Mpanda mkoani Katavi ambao wamehidhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo. (Picha na CCM Makao Makuu)





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments