DC TEMEKE JOKATE MWEGELO AKAGUA MIUNDOMBINU YA MASOKO

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika maeneo ya masoko waliyohamishiwa wafanyabiashara Wadogo maarufu Machinga, leo Novemba 10,2021 huku akiambatana na baadhi ya viongozi na wakuu wa idara za halmashauri ya manispaa ya Temeke.


Katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya amesisitiza kukamilishwa kwa miundombinu ya maji na matundu ya vyoo kwenye maeneo hayo ya kufanyia biashara ili kuweka mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara, na kuendelea kuvutia wengine waliopo maeneo yasiyo rasmi.

Hata hivyo Mhe. Jokate amewataka Watendaji na maafisa biashara wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanashirikiana na Serikali kuhamasisha wafanyabishara hao kutoka barabarani na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wao kufanya biashara.

“Haiwezekani Serikali inaweka mikakati mizuri ya kuwasaidia Wananchi,lakini watu wachache wanataka kukwamisha hili zoezi, kiukweli hatutawavumilia na tutawashughulikia” alisema Mhe. Jokate.

Naye afisa biashara wa manispaa ya Temeke Ndugu. Ramadhani Gurumukwa ametoa siku kumi na Nne (14) kuanzia leo, kwa Wafanyabiashara waliopewa vizimba katika maeneo rasmi kuhamia , na ikiwa watashindwa, baada ya siku hizo vizimba vyao watapewa Wafanyabiashara wengine ambao wako tayari kutii maelekezo.

Masoko yaliyotembelewa na Mkuu huyo Buza Sigara, Kanisani -Savoi, Mbagala Saku, Kiramba, Charambe na Mbande huku akikiri kuridhishwa na kazi inayofanywa na viongozi wa Wamachinga katika kuhimiza ufanyaji wa biashara kwenye maeneo yanayotambulika na Serikali,na kumuagiza kamanda wa polisi Temeke kuhakikisha vyombo vya usafiri wa Abiria vinafika katika vituo vilivyo jirani na masoko hayo,na sio kugeuzia njiani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments