Diarra, Djuma kuandika historia mpya Afrika

 IKIWA Mali na DR Congo zitafanya vizuri katika hatua ya mwisho ya mchujo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, kipa Djigui Diarra na beki Djuma Shaban wanaweza kuandika historia mpya ambayo haijawahi kuwekwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara tangu ilipoanzishwa.

Historia hiyo ni ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia wakiwa wanacheza katika Ligi Kuu Tanzania Bara jambo ambalo halijawahi kufanywa na mchezaji yeyote hapo nyuma.

Diarra ndio mwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kwenda Qatar ikiwa Mali itafanikiwa kufuzu Fainali hizo za Kombe la Dunia kwani licha ya kutopata nafasi ya kuanza kikosini amekuwa ni miongoni mwa makipa watatu ambao kocha Mohamed Magassouba amekuwa akiwaita katika kikosi chake.

Kipa chaguo la kwanza kwa Mali ni Ibrahim Mounkoro ambaye anachezea TP Mazembe ya DR Congo huku chaguo la pili akiwa ni Ismael Diawara ambaye anacheza soka la kulipwa huko Sweden katika timu ya Malmˆ.

Katika mechi sita zilizopita za kundi E ambalo Mali iliongoza, Kipa Mounkoro alidaka katika mechi tano huku Diawara akisimama langoni katika mechi moja wakati huo Diarra akisotea benchi.

Ukiondoa Diarra, Djuma naye anaweza kupata fursa ya kwenda katika Fainali za Kombe la Dunia ikiwa DR Congo itakuwa miongoni mwa timu tano zitakazopenya katika hatua ya mchujo.

Hata hivyo nafasi inaonekana kuwa finyu kwa Djuma kwani amekuwa haitwi mara kwa mara katika kikosi cha DR congo tofauti na ilivyo kwa Diarra.

Kocha Hector Cuper amekuwa akipendelea kumtumia zaidi beki Mukoko Amale anayechezea Difaa Jadida ya Morocco.

Hata hivyo Ligi Kuu Tanzania Bara imeshawahi kuwa na mchezaji aliyewahi kucheza Kombe la Dunia ingawa alishiriki mashindano hayo akiwa bado hajaanza kucheza katika Ligi yetu.

Mchezaji huyo ni kipa Daniel Agyei ambaye alikuwa katika kikosi cha Ghana kilichoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini na alisajiliwa na aliitumikia Simba katika msimu wa 2016/2017.

Kocha na nyota wa zamani wa Simba, Abdallah Kibaden alisema kuwa uwepo wa wachezaji kama Diarra unaongeza thamani ya ligi yetu.

“Mchezaji wa kigeni ni lazima awe na kitu cha utofauti na wazawa hivyo unapoona mchezaji anacheza katika Ligi ya Tanzania na anaitwa katika kikosi cha taifa kubwa kisoka kama Mali.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments