DITOPILE: RAIS SAMIA AMELETA MILIONI 800 NGORONGORO UJENZI WA MADARASA

Mbunge wa Viti Maalim Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewaomba wananchi wa Ngorongoro kumchagua Shangai awe Mbunge wa Jimbo hilo ili aweze kushirikiana na Serikali kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo iliyokua inatekelezwa na aliyekua Mbunge Ole Nasha.

Ditopile ameseam Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo na yeye kama Mbunge mwanamke atashiriki kikamilifu kuwaeleza wananchi makubwa yaliyofanywa Ngorongoro ili wamchague Shangai akaendelee kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

"Ndani ya Kipindi Kifupi Rais Samia Suluhu Hassan amewaletea Fedha hapa Ngorongoro zaidi ya Milioni 800 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa 40,kwa mara ya kwanza hamtachangishwa fedha za ujenzi wa madarasa ya Sekondari. Tuleteeni Emmanuel Shangai ashirikiane na Rais Samia kuwaletea Maendeleo.

Hapa Ngorongoro Wakati wa Msimu wa mvua takribani 60% ya barabara kuu ya wilaya na barabara zinazounganisha vijiji na vijiji zinapitika kwa tabu, Rais Samia amesikia kilio Chenu amewaletea Fedha Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Barabara na Madaraja, haya atayasimamia vyema Shangai mkimpa kura za kutosha.

Rais Samia pia hajaishia hapo tunajua huku ni Wafugaji na kuna Vijiji vipo mbali, Rais Samia amewaletea Fedha zaidi ya Milioni 560 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Shikizi 29 hapa Ngorongoro. Rais Samia anayo nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wana Ngorongoro" Amesema Ditopile.

Wananchi wa Jimbo la Ngorongoro wanafanya Uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Uwekezaji Ole Nasha.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments