Recent-Post

ENGLAND YAICHAPA 10-0 SAN MARINO NA KUFUZU KOMBE LA DUNIA NCHINI QATAR 2022

TIMU ya taifa ya England imefuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani Qatar baada ya ushindi wa 10-0 dhidi ya wenyeji, San Marino usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Olimpico Jijiji Serravalle.
Mabao ya Three Lions yalifungwa na Harry Maguire dakika ya sita, Filippo Fabbri aliyejifunga dakika ya 15, Nahodha, Harry Kane manne dakika za 27 kwa penalti, 31, 39 kwa penalti na 42.
Mengine yalifungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 58, Tyrone Mings dakika ya 69, Tammy Abraham dakika ya 78 na Bukayo Saka dakika ya 79.
Hii ni mara ya kwanza England Iliyo chini ya kocha Gareth Southgate inafunga mabao zaidi ya tisa kwenye mechi moja tangu mwaka 1964 na inamaliza na pointi 26 na kufuzu fainali za Qatar kama kinara wa Kundi I ikiizidi pointi sita Poland ambayo sasa itakwenda kujaribu bahati katika Playoffs.

Post a Comment

0 Comments