Kwani nyie hamumuogopi huyo Mayele!

Licha ya kuianza mechi kwa kupooza, lakini Yanga haikwenda mapumziko bure baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza kibabe ikiwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza.

Mchezo huo ambao unapigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa, Yanga walionekana kutawala mpira haswa kuanzia dakika 16 walipopata bao la kuongoza na kuwafanya wapinzani kuonekana kupaniki.

Hata hivyo kiungo mwenye pasi za macho, Feisal Salum ndiye alikuwa msaada mkubwa zaidi kwa kuhusika katika mabao hayo mawili kutokana na ufundi wake alivyokuwa akiwageuza wachezaji wa Mbeya Kwanza.

Bao la kwanza likifungwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya 16 kwa mpira a faulo baada ya Salum kuangushwa nje kidogo na eneo la hatari na nyota huyo kuukwamisha mpira wavuni.

Straika mwenye makeke mengi uwanjani, Mayele aliwainua mashabiki alipoifungia bao la pili Yanga dakika ya 25 kufuatia pasi safi ya Fei Toto na kuongeza ari na kujiamini kwa timu hiyo.

Hata hivyo kabla ya mabao hayo kupatikana, Yanga ilikosa umakini kwa kushindwa kutumia vyema nafasi mbili kupitia kwa Deus Kaseke aliyeshindwa kumalizia pasi ya Feisal dakika 18 na Mayele aliyekosa dakika ya kwanza alipopokea pasi ya faulo ya Ntibazonkiza.

Mayele alikuwa aipatie bao la tatu Yanga, lakini mwamuzi Abdulazizi Ally alikuwa makini kuona makosa yake kwa kuwa ameotea na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Yanga ikiongoza kwa mabao mawili hayo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments