MADIWANI KASULU WASHUHUDIA VAMIZI ULIOFANYWA NA WAKULIMA,WAFUGAJI HIFADHI YA MAKERE FOREST MAYOWASI

 

Wanyama waliokamatwa baada ya kuwindwa na majangili.
Meneja wa kitalu cha uwindaji Cha Makere na eneo la wazi uvinza , Shadrack Kagoma akionesha watu walivyovamia eneo la hifadhi na kulima Mpunga.

Mwandishi Wetu, Kasulu

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Kasulu Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo wametembelea eneo la Hifadhi ya Makere na eneo la wazi la ardhi oevu ambalo limevamiwa na Idadi kubwa ya wafugaji na wakulima.

Wakizungumza baada ya kutembelea eneo hilo la hifadhi leo Novemba 16,2021 ,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elia Charles  Kagoma  akiwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Joseph Rwiza wamesema wamesikitishwa na uvamizi huo na kwamba hatua za haraka zinahitajika.

Kagoma amesisitiza kwamba hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa na Mamlaka husika kwa kuweka mipaka eneo hilo kutenga eneo la hifadhi na eneo la vijiji ili iwe rahisi kuwaondoa wavamizi wote."Lazima kuwepo alama maalum kuzunguka eneo hili ambalo ni kitaku Cha uwindaji ili kuhakikisha uvamizi unakomeshwa".

Kwa upande wake Rwiza ametaka kuwepo na ushirikiano wa kupambana na wanaojihusisha na vitendo vya ujangili katika eneo hilo ambalo ni muhimu Kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza na viongozi hao wa halmashauri,Meneja wa  kitalu Cha uwindaji ncha Makere na eneo la wazi uvinza,Shadrack Kagoma amesema eneo hilo Sasa Kuna ujangili kutokana na uvamizi wa watu.

"Tuna wageni wa kimataifa wa uwindaji katika eneo hili lakini shida wakifika wanakuta kitalu chetu Kuna uvamizi wa Mifugo,kilimo na majangili"amesema.

Amesema wavamizi wakiwepo kutoka nchi jirani wanaingia Mifugo eneo la hifadhi na kulima na baadhi wanaojihusisha na ujangili.

Eneo la ikolojia Moyowasi-Malagarasi ni muhimu Kwa maslahi ya uhifadhi duniani na Taifa kwani kuna wanyama ambao hawapatikani sehemu nyingine.

Katika eneo hilo linalopakana na Ziwa Tanganyika pia Kuna ndege aina ya Korongo Nyangumi ambao hawapatikani sehemu nyingine Duniani na Kuna makundi makubwa  za Zohe statunga na Pofu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments