MASUMBUKO AAPISHWA KUWA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA

 

Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko ameapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga baada ya kuchaguliwa kwa kura za Ndiyo na Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021 huku akiahidi kuboresha ukusanyaji mapato, kudhibiti mianya ya rushwa ili kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kuimarisha nidhamu kwa watumishi wa umma. Masumbuko amepigiwa kura 20 za Ndiyo kati ya kura zote 20 zilizopigwa wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. Picha zote na Amos John 
Kushoto ni Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Kulia ni Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akienda kubadilisha Joho la Udiwani ili avae Joho la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko Kanuni za kuongoza Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. 
Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu  akimkabidhi Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko Ilani ya CCM leo Jumanne Novemba 30,2021. 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments