MBUNGE KAMONGA ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI

 Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ametembelea na kusaidia shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika kata mbalimbali wilayani humo uliotokana na fedha za uviko 19.


Mbunge huyo ndani ya siku mbili tayari ametembelea shule za sekondari zilizopo katika kata sita ambazo ni sekondari Kayao, Madilu, Lugarawa, Ikovo, Mundindi pamoja na shule ya sekondari mavanga na bado anaendelea na ziara yake katika kata nyingine zaidi.

Mbuge huyo amesema katika kata ambazo amedika amekutana na changamoto upatikanaji hafifu wa saruji ambapo kutokana na zoezi hilo la ujenzi kuwa la nchi nzima limepelekea saruji kupungua na kutopatikana kwa wakati.

Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kulipatia jimbo lake kiasi cha sh. bilioni 1,210,000,000 ambazo zimekuwa ni msaada na kuwapunguzia wananchi michango ya mara kwa mara.

Amesema fedha hizo zimelenga maeneo mbalimbali ambapo vyumba 47 vya madarasa sekondari sh. 940,000,000 bweni wanafunzi wenye uhitaji maalum sh. 80,000,000, vyumba vya wagonjwa ICU shs. 100,000,000 na nyumba ya mtumishi sh. 90,000,000

"Changamoto hizi za madarasa na vituo vya afya zipo maeneo mengi katika jimbo langu hivyo ujio wa fedha hizi zimesaidia kutatua changamoto hizi kwa wananchi wangu", amesema Kamonga.

Aidha kwa upande wa baadhi ya madiwani wa kata hizo wameishukuru serikali sambamba na kueleza juhudi walizonazo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi huo.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kushoto) akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Mundindi, kulia ni mwenyekiti wa halmashauri Wise Mgina pamoja na katibu wa vijana CCM Baraka Kalinga
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwaaga wanafunzi wa shule ya sekondari Ikovo baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kushoto)wakiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Baraka Karinga wakishiriki ujenzi wa vyumba vya Madara kwa kubeba mawe
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akichanganya mchanga na saruji katika shule ya sekondari Ikovo iliyopo kata ya Ludende wilayani Ludewa, kushoto ni katibu wa CCM vijana wilaya ya Ludewa

Na Damian Kunambi, Ludewa


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments