MBUNGE WA CHADEMA ACHACHAMAA BUNGENI KUHUSU DENI LA MSD

 

Na.Mwaandishi Wetu DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalumu Agnesta Lambert ( CHADEMA), amesema Bohari Kuu ya Dawa Nchini (MSD) ina hali mbaya kifedha hivyo amependekeza Serikali iwapatie Sh. billion 600 ili iweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Lambert ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mpango wa maendeleo wa mwaka 2022/2023 ambapo alisema MSD inahitaji mtaji mkubwa ili iweze kufanya shughuri zake vizuri.

” Mwenyekiti MSD ilikuwa ikiidai Serikali Sh. Billion 269, lakini baada ya Kamati ya PAC kupiga kelele Serikali iliipa MSD Sh. Billioni 39, hivyo ikabaki deni la Sh. Billioni 230″, alisema Lambert.

Mbunge huyo alinukuu kifungu alichosoma Waziri Nchemba katika UK. 14 na UK. 15 ambayo alisema upatikanaji wa dawa muhimu zilisambazwa katika vituo vya Afya kwa asilimia 94.

Alisema Waziri huyo aliendelea kusema Serikali ilitoa Sh. Billioni 234 kwaajili ya kununua dawa na Sh. Billioni 26.3 ya vifaa Tiba hiyo siyo halisi.

Mbunge huyo aliendelea kusema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seriki ( CAG) ilisema MSD ina Hali mbaya hivyo inahitaji kuongezwa nguvu.

Aidha Kamati ya Bajeti nayo ilisema MSD Ina hali mbaya hivyo ilipendekeza MSD ipewe Sh. Billioni 363.39 ili iweze kufanya kazi zake vizuri.

” Kwakweli Kamati ya Bajeti imenifurahisha kwa kazi nzuri,kwa kupendekeza MSD iongezewe fedha hizo yaani kwa msemo wa Sasa tunaweza kusema Kamati hiyo imeupiga mwingi”, alisema Lambert.

Pia Mbunge huyo aligongelea msumari wa mwisho kwa kusema hata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Oktoba 10 mwaka huu aliongea mbele ya vyombo vya habari na kusema huko Mikoani hali mbaya hivyo aliwapa Wiki moja MSD iwe imepeleka dawa Mikoani.

” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD na Naibu Waziri wa Afya aliongea kwenye vyombo vya habari baada ya kutoka kwenye ziara Mikoani alisema Mikoani hali mbaya dawa hakuna”, alisema Lambert.

” Kamati ya Bajeti ilipendekeza MSD ipewe shilingi Billioni 150 kati ya shilingi Billioni 363.39, ambayo ndio mahitaji halisi ya mtaji ili angalau iweze kutekeleza baadhi ya majukumu”

Hata hivyo, Mbunge huyo alisema kiasi hicho cha fedha kinachopendek zwa na Kamati ya Bajeti kupelekwa MSD (bilioni 150) ni kidogo mno ukilinganisha na mahitaji halisi ya mtaji. Aidha, badala ya kiasi hicho kuisaidia MSD kutekeleza majukumu yake, kitaiongezea STRESS kutokana mzigo mkubwa wa madeni.

Aidha, kutokana na kukinzana kwa taarifa ya Waziri wa Fedha iliyosema upatikanaji wa dawa na vafaa tiba nchini umefikia asilimia 94, huku taarifa za Kamati ya Bajeti, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na maelekezo ya Waziri Mkuu yakionyesha kuwa Kuna uhaba wa dawa na MSD iko hoi kifedha, Mbunge huyo aliitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu usahihi wa taarifa hizo!

“Mheshimiwa Mwenyekiti, tuamini taarifa ipi, hotuba ya Waziri wa Fedha, au taarifa za Kamati ya Bajeti na PAC au taarifa ya Waziri Mkuu? Mbunge huyo alihoji.

Aidha Mbunge huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alipendekeza Serikali katika fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia (IMF) sh. Trilioni 1.3, itoe Sh. billioni 600 wapewe MSD ili iweze kulipa madeni na fedha itakayobaki itumike Kama mtaji.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa, Serikali iweke kwenye mpango wa Maendeleo wa 2022- 2023 mkakati wa kulipa deni lake kwa MSD kwa mkupuo mmoja sambaba na kuipatia MSD mtaji wa kutosha ili iweze kuzalisha,kununua na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kulinda afya za watanzania

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments