NBAA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya huduma za Fedha Kitaifa alipokuwa anafungua maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja  kuanzia  tarehe 08 na hadi tarehe 14 Novemba 2021 yenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali na kutoa elimu Juu ya huduma za Fedha.

Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA) imeshiriki maonesho hayo ya Wiki ya huduma za Fedha Kitaifa ili kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu kazi na huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni  “Boresha Maisha kupitia elimu ya fedha.”

Maadhimisho ya wiki ya huduma za Fedha Kitaifa yameandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yaliyoanza  tarehe 08 na hadi tarehe 14 Novemba yenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali na kutoa elimu Juu ya huduma za Fedha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia Fedha kwanye mitaji ya wajasiariamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.

Amesema Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.

Akizungumza kwenye maonesho hayo Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya  amesema unapozungumzia huduma za Fedha huwezi kumwacha Mhasabu na Mkaguzi kwani wao ndio waandaaji na Wakaguzi wa Hesabu za Fedha.

Mwisho amewakaribisha wananchi na wadau wote wa Taaluma ya Uhasibu kutembelea banda lao katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupata elimu zaidi juu ya kazi na huduma mbalimbali zinazotolewa na NBAA.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa maelezo kwa Ngabo Nyamaseki kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa maelekezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NBAA kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa maelezo kwa Franco Kakurwa kuhusu gharama za mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa maelezo kwa Japhet Muluma namna anavyoweza kujiunga na Mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) hata kama hajasomea taaluma ya Uhasibu kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Maonesho yakiendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijjini Dar es Salaam

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments