Ndugai Awang’ata Sikio Wafanyabiashara Nchini

Spika wa Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw Job Ndungai watatu kushoto akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni Jijini Dodoma juzi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA, Bw. Nebart Mwapwele, Wapili kushoto ni Rais wa TCCIA, Bw. Paul Koyi, Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, Bw. David Kihenzile, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na wapili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Fatuma Mganga.
Rais wa TCCIA Bw Paul Koyi wa (Pili kulia) akimtambulisha Spika wa Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw Job Ndugai (kulia) wajumbe wa Bodi wa Chemba hiyo kwenye hafla fupi ya chakula jioni Jijini Dodoma juzi. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya TCCIA, Bi. Eutropia James Kushoto ni Bw. Swallah Swallah.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw Job Ndugai amewataka wafanyabiashara nchni kujenga tabia ya uwaminifu kwenye shughuli zao kama kigezo pekee kitakacho wajengea imani kwa Serikali na jamii ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Akizungumza kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Jijini Dodoma juzi,Spika Ndugai serikali inataka kuona sekta binafsi imara na inayokua lakini inazingatia uwaminifu na uwazi katika shughuli zake.

“Sisi kama Bunge tuna imani kubwa serikali inapenda sana kuona sekta binafsi inakua na kutoa mchango stahiki katika maendeleo ya taifa….lakini kitu pekee ambacho tunategemea kuona kutoka sekta binafsi ni kuonyesha uwaminifu na kuwa wawazi katika shughuli mnazofanya kwani kunabaadhi ya wafanyabiashara wamekuwa sio waaminifu,” alisema Spika Ndungai.

Mbali ya wito huo, Spika Ndugai aliwataka wafanyabiashara na wazalishaji kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vya hali ya juu ili bidhaa za Tanzania ziweze kushindana kwenye soko la dunia na kuweza kulipatia taifa fedha nyingi za kigeni sambamba na uchangiaji ukuaji wa uchumi.

“Sisi kama Bunge tupo tayari kufanya kazi na TCCIA kupitia Kamati yetu ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Tunapenda kuona sheria na sera mbalimbali zinasaidia kukuza na kuendeleza biashara na kukuza ucchumi hapa nchini,” alisema.

Alisema Dodoma ni mkoa wa kimkakati ambao unaweza kuwekeza kwenye kilimo, viwanda vya kusindika na biashara hivyo kuiomba TCCIA kuhamasisha wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo kuwekeza sambamba na azma ya serikali ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake, Rais wa TCCIA Bw Paul Koyi mbali ya kuishukuru serikali na bunge kwa kufanya kazi kwa kushirikiana, alisema TCCIA imekuwa mstari wa mbele katika kutoa ushauri wa namna bora ya kukuza mitaji kwa wajasiriamali, wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ongezeko la ajira.

“Nalishukuru sana Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kuonyesha imani kubwa kwetu (TCCIA) kama Chema tutaendelea kufanya kazi karibu na Kamati ya Bunge kwa manufaa na maslahi mapana ya taifa,” Alisema Bw Koyi.

Alisema TCCIA iliamua kufungua ofisi Jijini Dodoma ili kupunguza gharama wanazozitumia wanachama wake pamoja na wadau wengine kufuata huduma hizo Dar es Salaam sambamba na kuongeza ufanisi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Antony Mtaka alisema serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuinufaisha nchi pamoja na muwekezaji hivyo kupiti Ofisi yake ya Mkoa inawakaribisha sekta binafsi kwenda kuwekeza katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii .

‘’Kama serikali tunafanya kazi kwa karibu sana na sekta binafsi na tayari tulishaweka mazingira wezeshikupitia ofisi yangu ya mkoa. Tutatoa ushirikiano wakati wote tutakapo hitajika kwani Dodoma ni Jiji linalokua kwa kasi sana,” alisma RC Mtaka.

TCCIA ni taasisi ambayo imejipanga kumuinua mjasiriamali, mfanyabiashara wenyeviwanda na wakulima kwa kutoa ushauri wa kitaalamu wa namna bora ya kupata na kukuza mitaji yao sambamba kuchangia katika pato la taifa kwa kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments