Recent-Post

NEWZ ALERT: SIMBA SC YATAMBULISHA KOCHA MPYA

 WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC rasmi wametambulisha Kocha Mkuu mpya raia wa Hispania, Pablo Franco Martín ambaye aliwahi kuzifundisha timu za Real Madrid kama Kocha Msaidizi, mara ya mwisho kabla ya kutua Simba SC alikuwa akiifundisha timu ya Al-Qadsia SC ya Kuwait.


Kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, Simba SC imemtambulisha Kocha huyo siku chache baada ya kuachana na Kocha raia wa Ufaransa, Didier Gomes Da Rosa baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha hali iliyopelekea kutupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2021-22.

Kocha Pablo anakuja Simba SC ikiwa nafasi ya pili na alama 11 kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu huu wa 2021-2022, huku ikiangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC sasa itacheza na Red Arrows ya Zambia katika mchezo huo wa kuwania kufuzu Makundi ya Michuano hiyo.

Kocha Pablo mbali na kuiongoza Real Madrid kam Kocha Msaidizi, aliwahi pia kuziongoza timu za Getafe CF na Getafe B zote za Hispania, pia ameziongoza timu za Club Deportivo Santa Eugenia, Club Deportivo Illescas, Club Deportivo Puertollano zote za huko huko Hispania na FC Saburtalo ya Georgia.

Post a Comment

0 Comments