Recent-Post

Orodha ya majina ya vijana walioitwa kwenye usaili kwa ajili ya ajira katika Jeshi la Magereza

KUFUATIA ajira zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Kamishna Jenerali wa Magereza anawatangazia vijana walioomba ajira hizo kupitia makao makuu ya Jeshi la Magereza kwamba,kutakuwa na usaili wa vijana hao kuanzia Desemba 2,2021.


Usaili huo utadumu hadi Desemba 6,2021 katika Ukumbi wa Meja Jenerali SM Mzee uliopo makao makuu ya Jeshi la Magereza,Barabara ya Arusha eneo la Msalato, Dodoma.

Aidha, usaili huo utafanyika kuanzia saa mbili na nusu asubuhi. Gharama zote za malazi, chakula na nauli za kuja na kurudi katika usaili zitagharamiwa na wahusika.

Usaili huo umegawanywa katika makundi kulingana na taaluma za waombaji, orodha yao pamoja na tarehe ya usaili ni kama ifuatavyo;
NA MWANDISHI MAALUM

Post a Comment

0 Comments