PATO LA TAIFA KUPITIA SEKTA YA MADINI LAONGEZEKA

 


Na Mwandishi wetu - MichuziTv

WAZIRI wa madini Dkt.Dotto Biteko amesema kuwa miaka iliyopita kabla ya kufanyika kwa mabadiliko ya sekta ya madini mwaka 2017 ushiriki wa watanzania katika uchumi wa madini umeongezeka ndani ya kipindi cha mwaka 2020/2021 ambapo kampuni za watoa huduma kwenye migodi 961 sawa na asilimia 96 zilikua ni za kitanzania na idadi ya kampuni za kigeni zilikuwa asilimia 506 sawa na asilimia 34.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma katika mkutano wa waandishi wa habari wakati akieleza maendeleo ya sekta ya madini kabla na baada ya uhuru kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara.

Dkt.biteko amesema kuwa katika kuzingatia sera na sheria za madini nchini mapinduzi makubwa yamefanyika ambapo mpaka sasa serikali watanzania wananufaika na rasilimali madini kutokana na ongezeko la kasi ya ukuaji kutoka asilimia 17.7 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 27 mwaka 2020/2021.

Aidha waziri Biteko Amesema kuwa baada ya kuonekana kuwepo kwa changamoto kaadha katika sekta ya madini Serikali iliamua kufanya mapitio ya sheria mnamo mwaka 2010 kwa lengo la kuimarisha uwezo wa serikali katika kusimamia sekta ili iweze kuongeza mchango katika pato la taifa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments