Recent-Post

Paul na Peter Okoye wazua mjadala kundi la P-Square likitajwa kurejea

Kundi la P-Square kurejea. Unaweza kujiuliza swali hilo upendavyo kutokana na  wasanii wanaounda kundi hilo, Paul na Peter Okoye kuonekana tena pamoja.

Jana Jumatano Novemba 18, 2021 wawili hao walionekana  kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo Paul anaonekana akiingia ndani ya nyumba ya kifahari na kumfuata  Peter kisha kumkumbatia huku akiwa anamshagaa.

Pia, wapambe waliokuwa nao walionekana wakifurahishwa na kitendo hicho huku wengine wakisikika wakitaja jina la familia yao la  Okoye.

Kundi hilo kabla ya uvunjika mwaka 2015, lilijizolea umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali ikiwemo Beautiful Onyinye, Temptation, No One Like You na nyingine nyingi.

Chanzo cha kusambaratika ni malalamiko kutoka kwa Peter kutaka  mabadiliko katika uongozi kwa madai kaka yao Jude kuwa kiongozi, kundi lilionekana la kifamilia zaidi kuliko kibiashara.

Jambo hilo Paul hakuliafiki na hapo ndipo kikawa chanzo cha kundi hilo kuvunjika na kila mtu aliamua kufanya kazi kivyake ambapo Paul alianza kutumia jina la Rudeboy na kuanzisha lebo yake ya ‘Rudeboy’ huku  Peter yeye akijiita  Mr P na kutangaza uongozi wake mpya.

Post a Comment

0 Comments