Recent-Post

Picha : CCM YATOA MAFUNZO KWA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA WILAYA ZOTE TANZANIA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ndg Philip Japhet Mangula akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)

****
Chama Cha Mapinduzi leo Jumatano 3 Novemba,2021  Kimefungua mafunzo maalum ya watendaji wa Chama ambao ni Makatibu wa Mikoa na Wilaya zote nchini.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Philip Japhet Mangula katika ukumbi wa NEC makao makuu ya CCM jijini Dodoma.

Pamoja na Mambo mengine ya msingi  lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa katiba, kanuni na ilani ya Uchaguzi ya CCM, maelekezo ya vikao sanjari na masuala mbalimbali ya ujenzi wa Taifa letu.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku sita na zaidi ya mada 17 zitafundishwa na wakufunzi mbalimbali  waandamizi wa Chama na Serikali. 

Mafunzo hayo yatahitimishwa tarehe 6 Novemba,2021 ambapo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga Mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ndg Philip Japhet Mangula akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ndg Philip Japhet Mangula akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Christina Mdeme akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)

Post a Comment

0 Comments