MIRADI ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa nchi nzima imeleta neema na unafuu mkubwa kwa jamii.
"Kuna wafanyabiashara, wasafirishaji, wauzaji vifaa vya ujenzi madukani, wauzaji vifaa vya kujengea kama vile mawe, kokoto, mchanga na kuendelea, hawa wote wamepata neema ama fursa ya kufanya biashara, kujiongezea kipato kupitia utekelezaji ujenzi miradi hii ya elimu na mengineyo.
"Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tunamshukuru sana Rais Samia kwa miradi hii inayoenda kuondoa uhaba wa madarasa na pia amefanya mzunguko wa fedha uongezeke kwa jamii ambapo miradi hiyo inatekelezwa,"amesema Gavana Shilatu.
Tarafa ya Mihambwe imepata fedha toka Serikali Kuu shilingi milioni 420 kujenga vyumba vya madarasa 19 kwa shule za sekondari tano na vyumba madarasa mawili kwa shule shikizi moja.
Katika fedha hizo hizo pia wanajenga ofisi tisa za walimu na kuweka viti na meza kwenye madarasa hayo yote 21.
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
0 Comments