Samia ataka mitandao ya kijamii kutoa elimu usalama barabarani

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutumia mitandao ya kijamii kutoa elimu ya usalama barabarani na kushirikiana na vyuo vya usafirishaji kufanya tafiti ili kusaidia kupata suluhu ya kukomesha ajali barabarani.

Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama nchini yaliyofanyikia jijini Arusha leo Novemba 23, 2021 Rais Samia amesema licha ya kupunguza ajali za barabarani na kutoa vipindi vingi vya radio na runinga lakini ni muhimu elimu kutolewa kupitia mitandao pia.

Amesema kuna vijana hawasikilizi radio na kutazama runinga lakini wanasimu wanaweza kusikiliza elimu ya usalama barabarani.

Takwimu zenu mmesema  mmeongeza vipindi vya elimu kutoka 1625 mwaka 2020 hadi kufikia 2284 mwaka 2021 na vipindi vya runinga vimeongezeka kwa asilimia 47.8 rai yangu tumieni na mitandao" amesema

Mkuu huyo wa nchi amesema ni vyema Jeshi la Polisi likaendelea kujitahidi kutoa elimu kwa umma na askari wawe msaada kwa wananchi na sio kero ili kuweza kupata msaada wa kisheria za usalama barabarani.

Askari mjitahidi kuwa rafiki kwa watumiaji wa barabara na sio adui kwani  moja ya kero kwa askari wetu ni kuwataka madereva kulipa faini ya papo kwa papo ikiwa sheria haisemi hivyo,"amesema .

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments