SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING MABAO 3-1

 KLABU ya Simba imefanikiwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi ya NBC ukiochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mechi ilikuwa ya aina yake ambapo kocha mpya wa Simba Sc alikuwa na kibarua kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi na kufanikisha kuondoka na pointi tatu muhimu mbele ya maafande hao.

Katika mchezo huo Simba Sc ilianza kupata mabao matatu ya kuongoza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wao Kibu Dennis alifunga dakika ya 44 na Meddie Kagere ambaye amepachika mabao mawili dakika ya 17 na 36 kwenye mchezo huo.

Goli la kufutia machozi la Ruvu Shooting lilifungwa na Elias Maguli dakika ya 63.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments