Recent-Post

TANZIA: Mwenyekiti wa UVCCM Iringo C na Mjumbe wa Mtaa afariki

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Musoma Mjini mkoani Mara, Emmanuel Icon Nestory ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja huo tawi la Iringo C,Jama Ally Jama. You

Picha mbalimbali za Jama wakati wa uhai wake.

Kwa mujibu wa Nestory, kifo hicho kimetokokea leo Novemba 15,2021 saa tisa usiku.

"Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma (manispaa) umepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Mwenyekiti UVCCM tawi la Iringo C na mjumbe wa Serikali ya mtaa Iringo C ndugu Jama Ally Jama. Kilichotokea leo majira ya saa tisa xa usiku. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe. Amen,"ameeleza.

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Post a Comment

0 Comments