Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kilolo Frank Mbosa akiongea na waandishi wa habari wakati wa mahojiano maalum juu ya uelekeo wa jumuihiya hiyo wilayani Kilolo.
****************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Kilolo umewahimiza vijana kuwa na ujasiri wa kuwahoji na kuwakosoa viongozi Serikali badala ya kuwasifia hata katika Mambo yasiyo na tija Kwa Maendeleo ya Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Kilolo Frank Mbosa alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi kusifu Kila kitu kinachofanywa na viongozi wa chama au serikali kwa kufanya hivyo kumechangia kwa kiasi kikubwa baadhi viongozi kukengeuka na kutenda kinyume na maadili Utawala bora.
Mbosa alisema kuwa vijana wanajukumu la kusema ukweli,kusimamia serikali,kuonya na kuishauri serikali kwa mtazamo chanya ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa kwa kuwa wao ndio wanaonufaika zaidi kwa miaka mingi hapo baadae.
Alisema kuwa vijana hawatakiwi kuwa waoga kusema ukweli,kushauri au kufanya jambo jema kwenye majukumu ya kulitumikia taifa hili wanaweza kulitengeneza taifa ambalo litakuwa na vijana waoga kwenye ardhi yao na hatma ya maendeleo ya nchi hii.
Mbosa alisema kuwa vijana lazima wakatae vitu ambavyo wanaona kuwa sio kweli ni lazima vijana wakate kudanganywa kwa kuwa wao ndio wahanga wa muda mrefu sio watu wa kusifia kila kitu kinachosemwa na viongozi wa chama au serikali.
“Kuna wakati vijana wanasifia sana vitu ambavyo sio vya kweli utasikia safii sana wakati chafu sana au njema sana wakati sio njema kabisa hivyo vijana wanatakiwa kusema ukweli na kuwakosoa viongozi wanaowadanya vijana” alisema Mbosa
Alisema kuwa hata katiba ya chama cha mapinduzi kwenye ahadi namba nane (8) “inasema kuwa utasema kweli daima fitina kwangu mwiko” inawataka watu waseme ukweli wa mwenendo wa viongozi ambao wanawaongoza.
Mbosa aliwataka vijana hao kusema ukweli bila uoga kwa kufuata taratibu zilizopo bila kuvuruga amani iliyodumu kwa miaka mingi,lakini amewataka vijana kupaza sauti zao kwa mambo mabaya yanayosemwa na viongozi wao.
“ kwa mfano chama chetu tunautaratibu wa vikao kwa kusema ukweli bila woga kwa kuwa chama kinaona,kinasikia na kuyafanyia kazi mambo yote ambayo hayapo vizuri kwa maendeleo ya chama na serikali kwa ujumla” alisema Mbosa
Alisema kuwa chama cha mapinduzi kuna sehemu kimeyumba katika kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa hapo baadae kwa kuwa vijana wengi wa chama hicho wamekuwa wakusifia sifia tu bila sababu ya msingi hivyo vijana wa cha hicho wameanza kupoteza dira kutokana na kutopikwa vizuri kama ilivyo kuwa awali.
“Sijana wenye wamekuwa wa kusifia sifia viongozi wengi kwa sababu ya kupata manufaa ya muda mfupi maana vijana wengi iliwaonekane wa maana ni lazima wawasifie viongozi wakubwa ili wapate faida ambayo wameilenga” alisema Mbosa
Mbosa alisema vijana wengi wamejikita kwa ajiri ya kumsifia kiongozi furani kwa ajili ya kupata ajira kupitia mgongo wa kiongozi furani lakini sio kwa uwezo walionao tofauti na vijana wanaotoka vyama pinzani wamekuwa wanamisimamo kwenye ukweli wanasifia kwenye uongo wanakosoa hata vijana wa chama cha mapinduzi wanatakiwa kukosoa.
Alisema kijana ukiwa unasifia kila kitu mwisho wa siku yule ambaye unamsifia atakuona wewe ni kijana usiyekuwa na upeo wa mambo (kilaza),hivyo vijana lazima watumie ubunifu wao kupata ajira serikali au kwenye tasisi furani lakini kiwa ajili ya kumsifia mtu ndio upate ajira.
Vijana wengi wamekuwa waoga kukosoa viongozi kutokana na aina ya baadhi ya viongozi ambayo wanaongoza chama au serikali kuendelea kuzilinda nafasi zao licha ya kuwa kwenye nafasi hizo hawatoshi hivyo wanaogopa wakikosolewa wataondolewa madarakani.
Kiongozi huyo wa UVCCM Wilayani Kilolo ametoa Wito kwa viongozi waliopo madarakani katika vyama vyaSiasa na Serikali kukubali kukosolewa, akiitaja hatua Hiyo itawasaidia kujisahihisha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.
Mbosa alimalizia kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kipindi kifupi kuongeza ajira kwa vijana,kuwapandisha madaraja watumishi wa serikali,kuboresha miundombinu ya elimu kwa ujenzi wa madarasa,sekta ya afya kaiboresha pia,miundombinu ya barabara inaendelea kwa kasi katika wilaya ya Kilolo.
Aliwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo katika kila sekta hapa nchini.
0 Comments