UWT Wahubiri Upendo Ndani Ya CCM Ili Kuimarisha Chama

Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT) mkoa wa Njombe imetoa wito kwa wanawake wa jumuiya hiyo kuongeza amani,upendo ni mshikamano ndani ya Jumuiya ili kulinda na kukuza Chama chao.Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi.Scolastika Kevela ametoa rai kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa jumuiya katika wilaya ya Ludewa wakati kamati ya utekelezaji UWT ilipotembelea katika wilaya hiyo kwa lengo la kukagua miradi na kuimarisha uhai wa jumuiya.


“Chama hiki tunakilea sisi akina mama,tukahimize ustawi wa Chama cha mapinduzi na jumuiya kuanzia kwennye matawi,rafiki wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe tupendane na tufichiane madhaifu kwa kuwa hakuna mkamilifu”alisema Bi,Scolastika Kevela


Aidha amesisitiza wanawake kuongeza vipato vyao ili kukuza uchumi wa Jumuiya na Chama ili kupunguza vitendo vya rushwa.


“Tukiwa na uchumi hakutakuwa na haja ya rushwa,akina mama tusifike mahara sisi kuwa ni wa kununuliwa kwa kuwa tukiendelea kununuliwa tutachagua viongozi ambao wanaweza kutupoteza na pia ninasisitiza tulipe ada kwa kuwa Njombe tunatia aibu”aliongeza Scolastika Kevela.


Naye mjumbe wa baraza taifa UWT mkoa wa Njombe Bi,Anna Mwalongo ametoa wito kuongeza ushirikiano ili kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja na Chama.


“Sisi ni madaraja kwa hiyo tukikaa tu maana yake kutakuwa kuna kazi hatufanyi,tunaomba mtutumie ili mtoke mlikokuwa na mpande ngazi nyingine hata iwe kwa uchumi wako binafsi”alisema Anna Mwalongo


Bakari Mfaume ni katibu wa CCM wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambaye alikuwa katibu wa Chama hicho wilaya ya Ludewa aliyehamishwa hivi karibuni.Ametumia nafasi hiyo kuwaaga jumuiya ya wanawake (UWT) wilaya ya Ludewa kwa kuwasisitiza kuulinda uhai wa Chama kwa wivu mkubwa.


“Kinachotukutanisha ni Chama,kama chama hakina nguvu na hakipo hai basi makutano yetu yatakuwa hayana faida yeyote kwa hiyo ni vizuri muendelee kukijenga Chama kwa nguvu zenu zote na mwenyekiti wa Chama anataka Chama kinachotembea”alisema Mfaume


Nao viongozi wa jumuiya hiyo wameahidi kujenga mshikamano zaidi utakaowawezesha kulinda tunu na rasilimali za Chama na Jumuiya kwa lengo la kuendelea kufikia ndoto na matarajio ya Chama.


Kamati hiyo ya utekelezaji imefanikiwa kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya jumuiya wilaya ya Ludewa ukiwemo shamba la Parachichi na miti yaliyopo kijiji cha Mangalanyene kata ya Madope pamoja na kiwanja kilichopo Ludewa.

Baadhi ya wananchama wa Chama kutoka UWT wilaya ya Ludewa wakisikila kwa makini maagizo ya kamati ya utekelezaji walipofika katika wilaya ya Ludewa.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi.Scolastika Kevela akifundisha ujasiliamali wa ufugaji wa kuku kwa viongozi wa UWT wilaya ya Ludewa ili kusaidia kukuza vipato vya wananchama.
   Na Amiri Kilagalila,Njombe

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments