VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUUNGA MKONO SERIKALI KUHAMASISHA JAMII KUHUSU KUPATA CHANJO YA UVIKO 19

Viongozi wa dini wametakiwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha jamii kuhusu chanjo dhidi ya maambuziki ya ugonjwa hatari wa korona ikiwa ni sehemu ya kupambana na janga hilo.

Hayo yameelezwa na imamu wa msikiti wa Zahara, Maulidi  Sombi katika maadhimisho ya Maulidi yaliyofanyika hivi karibuni katika eneo la Makumbusho jijini Arusha ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa Kwa mtume Mohammad ambapo alidai lengo la Maulidi hayo Kwa mwaka huu ni kufufua mioyo ya Watu ili kurejesha mshikamano na upendo.

Sombi alisema kuwa jamii inapaswa kushiriki vyema katika zoezi la sensa hapo mwakani kuomba waumini kote nchini walio na dini na wasio na dini kushirikiana na serikali katika kufanikisha zoezi hilo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa watanzania kujulikana idadi kamili

Naye Naibu Katibu mkuu jumuiya ya Maridhiano Tanzania,Abdulazack Amiri alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuhimiza maadili mema Kwa waumini na Jamii Kwa ujumla kuepua kujiingiza katika matendo maovu yesiompendeza mwenywzi mungu.

Kwa upande wake sheikh Mlewa shabani Kimwaga kutoka Mkoani Kilimanjaro alisema kuwa maadhimisho ya Maulidi yanalenga  kuikumbusha Jamii kuhusu malezi Bora Kwa Jamii na watoto ikiwa ni njia sahihi ya kumwenzi mtume Mohammad

Nao waumini walio udhuria maadhimisho hayo walisema wamefuraishwa na mafundisho yaliotolewa na viongozi hao wa dini kwani kwa sasa ni kweli jamii imekosa maadili na kusau dini 

Waliongeza kuwa watahakikisha wanaunga mkono serikali juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa corona

Imamu wa msikiti wa Zahara,Maulidi Sombi akizungumza katika maadhimisho ya Maulid yaliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni
Viongozi wa dini wakifuatilia maadhimisho ya Maulid yaliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni.
  Na Pamela Mollel,Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments