Recent-Post

Wafuasi Simba SC wataka mambo mawili kwa Pablo

Wafuasi wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania mara nne mfululizo, wameanza kuelekeza macho na masikio kwa Kocha wao mpya, raia wa Hispania, Pablo Franco Martin huku wakihitaji kuona mambo mawili yanafanyiwa kazi haraka.

Kwa nyakati tofauti wameieleza DIRAMAKINI BLOG kuwa, mambo ambayo wanataka kuona yanabadilishwa haraka na kocha huyo mpya ni pamoja na kuona safu ya ulinzi inaimarishwa ili kuwezesha mabingwa hao kusonga mbele zaidi.

Pia wamesema, wanataka kuona upande wa uokoaji mwalimu anaimarisha upande huo, kwani mambo hayo mawili yamekuwa miongoni mwa changamoto kubwa katika kikosi.

Rai hiyo inakuja ikiwa tayari Kocha huyo ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na Simba SC ameanza kazi rasmi Novemba 12, 2021 ikiwa wanajiandaa katika mechi zijazo.
Pablo mwenye umri wa miaka 41 alichukua nafasi ya Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake na Simba SC ulisitishwa hivi karibuni baada ya makubaliano ya pande mbili.

Raia huyo wa Hispania na mzaliwa wa Madrid, kabla ya kujiunga na Simba SC alikuwa anafundisha timu ya Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Pia Pablo mwenye umri wa miaka 41 mwaka 2015 alikuwa kocha wa Getafe inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania na pia alikuwa kocha Msadizi wa Real Madrid mwaka 2018 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadae Santiago Solari.
 Kocha mpya wa Simba SC, Pablo Franco Martin akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa mazoezi Novemba 12, 2021.
NA GODFREY NNKO

Post a Comment

0 Comments