WAKONGO WAICHAPA TAIFA STARS 3-0 NYUMBANI, MATUMAINI QATAR NJIA PANDA

 TIMU ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' imekubali kipigo cha mabao 3-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam mbele ya DR Congo na kuweka njia panda matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Qatar.


Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa Tanzania ambayo ilikuwa inaongoza kundi J ikiwa na alama 7 sawa na Benin, huku Congo wakishika nafasi ya tatu na alama zao tano wakifuatiwa na Madagascar waliokuwa na pointi 3, ambapo endapo Tanzania ingeshinda ingejiweka katika mazingira mazuri na kwenda kumalizia mchezo wa mwisho dhidi ya Madagascar ugenini Novemba 14.

Mabao ya DR Congo yalifungwa na Gael Kakuta dakika ya sita, Nathan Fasika dakika ya 70 na Ben Malonga mnamo dakika ya 85 na kufanya wawe vinara wa kundi hilo wakifikisha alama 8 huku Tanzania ikisalia na pointi zake saba.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments