Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za mitaa, Abdallah Chaurembo, aliwataka wananchi kuendelea kujitoa kutekeleza miradi mbalimbali inayo tekelezwa na Serikali yenye lengo la kuwaletea maendeleo
Hii ni baada ya kusomewa taarifa ya utekelezwaji wa miradi ya TASAF ambapo ilielezwa kuwa wakazi wa eneo Hilo wamechangia Katika ujenzi wa shule ya Sekondari Oldonyowas
Akiongea Katika Kijiji hicho cha Oldonyowas wilayani Arumeru, wakati wa kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za mitaa ilipotembelea shule ya Sekondari Oldonyowas, alisema kuwa wananchi wamejitoa kwa kuchangia mradi huo
Fedha hizo zimetumika kukamilisha Madarasa mawali, nyumba mbili za walimu,mabweni mawili na jengo la Utawala Katika shule hiyo
Kwa upande wake,Waziri wa nchi ofisi ya Rais,Utawala Bora , Mohamed Mchengerwa amewataka Wananchi kuhoji matumizi ya mamilion ya fedha yaliyopelekwa katika maeneo yao na serikali kwani ni haki yao .
Alisema Serikali ya awamu ya sita inatoa fedha nyingi katika halmashauri hivyo Wananchi wasisite kutumia haki yao kwenda ofisi za halmashauri kuwauliza wakurugenzi matumizi ya fedha.
"Wananchi mnahaki ya kuuliza miradi yote inayofanyika Katika maeneo yenu ili mjue , thamani ya miradi kuepusha matumizi mabaya ya fedha,,alisema
Alisema kuwa serikali imetoa sh 130 bilioni Kwa mikoa mitano ilikukabiliana na kutatua changamoto za Wananchi katika kuondoa ujinga,umasikini na kupambana na maradhi.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo upo katika utekelezwaji wa miradi ya awamu ya nne na kutaja mikoa ambayo itanufaika ni Arusha,Geita,Simiyu,Mwanza na Njombe.
" Tunataka miradi yote itekelezwe kwa uadilifu na kwa wakati katika Maeneo ambayo yatapata fedha" amesema
Mradi wa mfuko wa maendeleo ya jamii, TASAF unatajwa kuisaidia jamii hususani kaya maskini baada ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo elimu, Afya pamoja na mitaji ya biashara ndogondogo za kilimo na ufugaji.
0 Comments