WANAOKUSANYA NA KUTUMIA TAARIFA ZA WATU BINAFSI KUPITIA MITANDAO WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi akihutubia kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Ashatu Kijaji wakati akifungua Mkutano wa nane wa masuala ya usimamizi wa mtandao Tanzania (TZIGF) ulioandaliwa na Taasisi ya Internet Society (ISOC) Tanzania Chapter na kufanyika katika hoteli ya Protea, Courtyard, Dar es Salaam.


Rais wa Shirika la Internert Society Tanzania na Mratibu wa jukwaa la usimamizi wa intaneti Tanzania Nazar Nicholas akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa masuala ya usimamizi wa mtandao Tanzania (TZIGF) ulioandaliwa na Taasisi hiyo ya Internet Society (ISOC) Tanzania Chapter na kufanyika katika hoteli ya Protea, Courtyard, Dar es Salaam.




* ISOC yapongezwa kwa kuwakutanisha wadau na kutoa elimu kuhusu matumizi chanya ya mitandao

SERIKALI imewataka wanaokusanya na kutumia taarifa za watu binafsi, taasisi na Serikali kupitia mitandao kutimiza wajibu wao kwa kuzilinda kwa kufuata kanuni, taratibu, sheria, maadili na nidhamu ya kulinda taarifa hizo kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuzilinda taarifa hizo.

Hayo yameelezwa leo na Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi wakati akifungua mkutano wa nane wa wa masuala ya usimamizi wa mtandao Tanzania (TZIGF,) ulioandaliwa na Taasisi ya Internet Society (ISOC,) na kuwakutanisha wadau wa mtandao wakiwemo watafiti, wakufunzi, wanafunzi wa vyuo na kueleza kuwa, matumizi ya intaneti ni muhimu kwa jamii lakini lazima ithibitiwe kwa watumiaji kufuata kanuni na taratibu kwa kufuata kanuni, taratibu na miongozo.

Yonazi amesema mkutano huo watajadili sera ya usimamizi wa mtandao na namna na bora ya matumizi ya mtandao pamoja na fursa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi na kijamii zinazopatika kupitia matumizi ya mtandao hasa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya UVIKO-19 ambapo fursa zaidi zimefunguka.

''Matumizi ya mtandao ni haki kwa watu wote ila yazingatie nidhamu, maadili na kufuata kanuni na taratibu.....kuna fursa nyingi hasa kwa vijana na uwepo wa mitandao mbalimbali ya kijamii imeleta ushindani mkubwa katika taasisi na watu binafsi katika biashara ni vyema makundi yote kutumia fursa hiyo kwa kuleta mafanikio chanya zaidi.'' Amesema Yonazi..

Amesema kutokana na umuhimu wa matumizi ya mtandao Serikali inachukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma hiyo.

''Katika kuhakikisha kwa hili Serikali imewekeza na inajenga mkongo ili huduma hii iweze kufika katika maeneo mbalimbali ya taifa letu pamoja na kuhakikisha gharama inashuka na upatikanaji wa huduma hiyo unakuwa wa uhakika.'' Amesema.

Amesema, Serikali imeendelea kuwahimiza wawekezaji kuwekeza katika mikongo ya bahari na mpango wa ni Serikali ni kuwafikia wananchi katika mikoa yote nchini kwa gharama nafuu na uhakika zaidi na imeipongeza taasisi ya ISOC kwa jitihada zao za kuhakikisha elimu ya matumizi sahihi ya mtandao inawafikia wananchi hususan vijana

Kwa upande wake Rais wa Shirika la Internert Society Tanzania na Mratibu wa jukwaa la usimamizi wa intaneti Tanzania Nazar Nicholas amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha wadau wa jukwaa la masuala ya mtandao kwa wiki moja na kujadili masuala mbalimbali ya mtandao ikiwemo sera na majadiliano, mapendekezo na makubaliano yatapelekwa kwa Serikali ha hatua zaidi.

Nazar amesema wataendelea kushirikiana na Serikali na wapo pamoja nayo katika kuhakikisha huduma ya mitandao unapatikana kwa watu wote na kwa gharama nafuu na kuutumia kwa faida.
























Matukio mbalimbali katika mkutano huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments