Watanzania waendelea kuchanga kujikinga na Uviko-19

Dodoma. Watanzania 88,546 wamechanjwa dozi ya kwanza ya Sinopharm ambayo ni sawa na asilimia 8.3 ya chanjo zote zilizosambazwa.

Idadi hiyo imetajwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jiinsia, Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi.

Profesa Makubi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akizindua mpango harakishi na haraka wa awamu ya pili wa chanjo ya Uviko-19 ambao unalenga kuwafikia Watanzania kwa asilimia 60.

Uzinduzi huo umekwenda sambamba na kutathimini utekelezaji wa vipaumbele vya sekta ya afya kwa mwaka 2020/21 ikiwemo programu ya dunia ya COVAX facility, ambapo Tanzania imetengewa chanjo 12,049,827. 

Profesa Makubi amebainisba kuwa Oktoba 8, 2021 Serikali ilipokea chanjo 1,065,600 za Sinopharm kama kundi la pili kutoka programu ya COVAX facility. 

"Utolewaji wa chanjo ya Sinopharm ulianza Oktoba 12, 2021 ambapo mpaka sasa watu 88,546 wamepokea dozi ya kwanza ya Sinopharm ambayo ni sawa na asilimia 8.3 ya chanjo zote," amesema Nchemba.

Amesema Tanzania inazingatia chanjo kama moja ya afua muhimu ya kudhibiti janga hilo ili kuendana na Mpango wa Kitaifa ambao unapendekeza matumizi ya chanjo ya Uviko-19 kama sehemu ya afya za kuzuia janga hilo.

Kuhusu chanjo ya Jonseen iliyopokelewa Julai 24, 2021, amesema jumla ya dozi 1,058,400 zilipokelewa ambapo hadi  kufikia Oktoba 19, 2021 watu 949,377 wamechanjwa ambayo ni asilimia 10 ya chanjo ya Janseen.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments