Watanzania wasuasua ulaji wa samaki

Baadhi ya watanzania nchini wamekuwa na tatizo la ulaji mdogo wa samaki hatua inayosababisha kukosa protini ya asilimia 30 inayopatikana katika kitoweo hicho.

Akizungumza wakati wa tamasha la ulaji wa samaki na dagaa, lililofanyika mjini Kigoma, ofisa mfawidhi usimamizi wa rasilimali za uvuvi kanda kuu ya ziwa Tanganyika, Juma Makongoro amesema watanzania wengi wamekuwa wavivu wa kula samaki mara kwa mara.

Amesema watanzania wamekuwa wakila samaki kilo 8.5 kwa mwaka badala ya kilo 22.8 ambapo hakuna sababu ya msingi ya wao kushindwa kula kitoweo hicho.

“Ni jukumu la kila mtanzania kushiriki katika kupiga vita uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi, na kwamba tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa maeneo ya vijiji ili kuhakikisha rasilimali hizo zinalindwa,”amesema Makongoro.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Easter Mahawe amesema kuna upotevu mkubwa wa mapato yanayotokana na mazao ya uvuvi kutokana na utoroshaji mkubwa wa mazao hayo kinyume na taratibu.

Amesema kuna mianya mingi ya utoroshaji wa mazao ya uvuvi na kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wamekwepa kufanya wajibu wao na kuhakikisha hili tatizo la utoroshaji linakwisha.

Mkurugenzi wa programu ya Tuungane, unaosimamia rasilimali za nchi kavu na za majini, Lukindo Hiza amesema uvuvi unachangia asilimia 35 ya ajira za watanzania hususani wanaoishi vijijini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments