WAZIRI MKUU AZINDUA TAMASHA LA MVINYO DODOMA

 


*Asisitiza miche ya zabibu za matunda izalishwe kwa wingi


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua tamasha la mvinyo mkoani Dodoma na kusisitiza kuwa uzalishaji wa miche ya zabibu za matunda uongezwe ili wajasiriamali wapate bidhaa kutoka mkoa huo.

“Hizi zabibu zinazouzwa barabarani siyo za kula kama matunda, hizo ni za mvinyo. Tuweke juhudi ya kuzalisha miche ya zabibu za mezani ili wajasiriamali wanaouza zabibu kwenye stendi za mabasi wapate bidhaa kutoka hapa Dodoma,” amesema.

Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Novemba 5, 2021) wakati akizungumza na wananchi na wadau wa zao hilo waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha la mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. Tamasha hilo litaendelea hadi Jumapili, Novemba 7, mwaka huu.

“Tunataka miche ya zabibu kwa ajili ya mvinyo na ile ya kula izalishwe kwa wingi. Hivyo, Mamlaka za Serikali za Mitaa itenge maeneo ya kuzalisha miche bora na kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) ili kuongeza uzalishaji na kurahisisha utoaji wa huduma za ugani, mitaji na upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya mvinyo.

Pia amezitaka Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zishirikiane na Wizara ya Kilimo kusimamia mikataba ya kilimo inayosainiwa baina ya wakulima, wanunuzi wa mazao na watoa huduma wengine ili kuhakikisha wakulima hawadhulumiwi.

Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo iratibu maonesho ya zabibu ili tamasha hilo liwe rasmi. “Mratibu wa tamasha hili, Bi. Atwite Makweta asaidiwe na wizara kusimamia maandalizi na kuanzia sasa haya maonesho yawe ya kudumu na yafanyike kila mwaka hapa Dodoma.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Anthony Mtaka kabla ya mwisho wa mwezi huu wakutane na wadau wa zao la zabibu wakiwemo wazalishaji, wasindikaji, wakulima na wenye viwanda na waibue mdahalo kuelekea miaka 60 ya Uhuru.

“Katika hili, mkae na muangalie kwenye zao la zabibu tumetoka wapi, tuko wapi na tunaenda wapi. Nini kifanyike ili kuimarisha zao hili, na hilo liende sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ambayo uzinduzi wake utafanyika hapa Dodoma tarehe 2 Desemba, 2021” amesema.

Mapema, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo P. Pinda alisema anaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi wake wa kulifanya zao la zabibu liwe miongoni mwa mazao nane ya kimkakati hapa nchini.

“Zao hili ni fursa kwa Dodoma na Taifa kutokana na upekee wake hapa nchini. Kwa hiyo kuna haja ya kuwaita wadau na kuwaelezea zao la mkakati maana yake ni nini na wananchi tutegemee nini katika jambo hili,” amesema.

Naye Waziri wa Kilimo, Prof. Mkenda alisema ili kuimarisha zao la zabibu, wizara hiyo imetenga sh. milioni.







TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments