Recent-Post

Yanga SC yatembeza kichapo Zanzibar

Wachezaji wa Yanga SC inaonekana wanaendelea kumuelewa mwalimu wao kwa haraka, hali ambayo inadhirisha wazi kuwa, wamekusudia kuwapa raha wafuasi wao.


Chini ya kocha Nasreddine Nabi Mohamed, Novemba 12, 2021 wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya KMKM katika mchezo wa kirafiki uliochezwa dimba la Amaan jijini Zanzibar.
Licha ya KMKM kutangulia kwa bao la Optatus Lupekenya dakika ya 20, kabla ya Yanga kuzinduka kwa mabao ya Wakongo ambao wamezidi kuwa mwiba akiwemo winga Jesus Moloko 27 na Fiston Mayele waliofanya kweli dakika ya 85.

Huu unakuwa mtanange wa pili wa kirafiki kwa Yanga SC baada ya Jumanne kushinda 1-0 hapo hapo Amaan, bao la Mkongo mwingine, Heritier Makambo.

Wanajwangwani hao waliwasili Jumanne jijini Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kipindi hiki cha mapumziko mafupi kupisha mechi za kirafiki na mashindano mengine.

 NA MWANDISHI DIRAMAKINI


Post a Comment

0 Comments