Recent-Post

Yanga yamnogea Kibwana

 

BEKI wa Yanga, Kibwana Shomari amesema maisha ndani ya Yanga kwa sasa ni ya furaha tofauti na msimu uliopita ambao walikuwa wanapambana kusaka matokeo. Lakini ametamka kitu kuhusu Ruvu Shooting.

Kibwana alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na sasa anamebakiza miezi saba kuitumilia timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti ambalo ndilo gazeti pekee la michezo la Kiswahili linaloongoza Kenya na Tanzania, alisema; “Tumecheza michezo mitano yote tuliichukulia kama fainali tunashukuru Mungu tumepata matokeo katika michezo hiyo ni Ruvu Shooting pekee wametupa changamoto.

“Kwanza sisi tulicheza mechi hatukupumzika hata siku tatu, tumecheza tena uchovu bado ulikuwepo lakini kwenye mpira ni kawaida kuna muda timu pinzani itakuwa ngumu, kikubwa ni kumsikiliza kocha nini anataka tufanye,” alisema.

Kibwana alisema Ruvu Shooting walikuwa bora zaidi eneo la ukabaji, waliwanyima mabao zaidi ya matatu waliyotengeneza na kusisitiza kuwa kipa wa Shooting, Mohammed Makaka alikuwa bora zaidi.

Akizungumzia msimu uliopita alisema ulikuwa na changamoto kwao kutokana na kukosa wachezaji wenye ubora kama walivyo sasa.

Post a Comment

0 Comments