Recent-Post

Zungu awapiga kijembe kijanja Yanga SC

Niwapongeze watu wote, hii inaonyesha demokrasia ndani ya Simba. Kama kuna wachezaji wapya watakuja leo mtuambie ni muhimu sababu nia ipo uwezo upo na pesa ipo;

Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 2021 wa Klabu ya Simba SC ameyasema hayo Novemba 21, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam (JICC).

Zungu ambaye ni pia ni Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Bungeni amesema hayo wakati akitoa hotuba ya dakika 15 mbele ya zaidi ya mashabiki 800 ambapo walijitokeza katika mkutano huo .

Pia amesema, Simba SC ni klabu kubwa na baadhi ya watu wanaamini timu yao ndiyo ilishiriki kwenye Uhuru wa Tanganyika, jambo ambalo halina ukweli.

Hao hawajui historia ya nchi yetu, eti klabu yao imeshiriki kwenye Uhuru,” alitania Zungu huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wa klabu hiyo.

Amesema viongozi waandaamizi wa Serikali akiwemo aliyekuwa waziri mkuu, Rashid Mfaume Kawawa walikuwa ni wanachama wa klabu hiyo walioshirikiana ipasavyo na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wacha wajisifu tu, lakini Taifa letu ni moja na Mwenyezi Mungu ni mmoja, lakini hawafahamu historia. Maneno yalikuwa mengi ulipoteuliwa kuwa CEO, lakini umeonyesha unaweza na sasa wewe ni CEO uliyekubuhu, usiogope vijembe na maneno hayo yapo tu,”amesema Mheshimiwa Zungu.

CHANZO NA    DIRAMAKINI

Post a Comment

0 Comments