Bodi yaingilia kati ishu mastaa wa Simba kuugua ghafla

Bodi ya Ligi (TPLB) imeamua kutuma jopo la madaktari, chini ya Dk Kaja, kwenda Kagera ili kuthibitisha kama kweli wachezaji wa Simba wanaumwa kabla ya kutoa maamuzi ya kuahirisha mchezo dhidi ya Kagera.

Inadaiwa maamuzi hayo yametokana na taarifa kwamba wachezaji sita waliougua waliachwa Dar tofauti na maelezo yanayotolew na Simba kuwa wachezaji 13 waliopo Kagera wanaumwa, japo Jonas Mkude na Hassan Dilunga  ndio wanaelezwa wameugua gafla wakiwa mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments